Matthew 21:1-6

Isa Anaingia Yerusalemu Kwa Shangwe

(Marko 11:1-11; Luka 19:28-40; Yohana 12:12-19)

1 aWalipokaribia Yerusalemu, wakafika Bethfage katika Mlima wa Mizeituni. Ndipo Isa akawatuma wanafunzi wake wawili, 2akawaambia, “Nendeni katika kijiji kilichoko mbele yenu, nanyi mtamkuta punda amefungwa hapo, na mwana-punda pamoja naye. Wafungueni na mniletee. 3 bKama mtu yeyote akiwasemesha lolote, mwambieni kwamba Bwana ana haja nao, naye atawaruhusu mwalete mara.”

4 cHaya yalitukia ili litimie lile lililonenwa na nabii, akisema:
5 d“Mwambieni Binti Sayuni,
‘Tazama, mfalme wako anakuja kwako,
ni mnyenyekevu, naye amepanda punda,
juu ya mwana-punda, mtoto wa punda.’ ”

6 eWale wanafunzi wakaenda, wakafanya kama Isa alivyokuwa amewaagiza.
Copyright information for SwhKC